Hatimaye baada ya mazoea ya ushindi wa kila mechi, wanaume wanaoongoza ligi ya Spain 'Barcelona' na mtabe wao Messi wamekanyaga sumari la moto; walipokubali kichapo cha 3-2 kutoka kwa Real Sociedad. Hii ikiwa ni mara ya kwanza katika msimu wa La Liga kwa watabe hawa kufungwa. Kama Kawida yao, Messi alianza kuzifumania nyavu akipokea pasi kutoka kwa Andres Iniesta na baadaye Pedro aliunganisha cross ilotoka kwa Dani Alves na kufanya mpaka mapumziko Barcelona waongoze 2-0. Katika kipindi cha pili, winga wa Uruguay 'Gonzalo Castro' alifumania nyavu na kuipa timu yake goli la kwanza. Castro alitwanga bao la pili baada ya Pique kupata kadi ya pili ya njano na kutolewa. Katika dakika za lala salama, Agirretxe aliteleza kumalizia mpira na kuwapa ushindi Real Sociedad wa 3-2. Hii ni timu ya tatu kutoa kichapo kwa Barcelona. Inaungana na Real Madrid katika 'Super Cup' ya Spain na Celtic kwenye 'champion league'.
jana pia wametoa draw na valencia
ReplyDelete