Video and Shared space for ads

CF

Sunday, January 20, 2013

Messi na Barcelona yake walakichapo kwa Real Sociedad katika La Liga

              Hatimaye baada ya mazoea ya ushindi wa kila mechi, wanaume wanaoongoza ligi ya Spain 'Barcelona' na mtabe wao Messi wamekanyaga sumari la moto; walipokubali kichapo cha 3-2 kutoka kwa Real Sociedad. Hii ikiwa ni mara ya kwanza katika msimu wa La Liga kwa watabe hawa kufungwa. Kama Kawida yao, Messi alianza kuzifumania nyavu akipokea pasi kutoka kwa Andres Iniesta na baadaye Pedro aliunganisha cross ilotoka kwa Dani Alves na kufanya mpaka mapumziko Barcelona waongoze 2-0. Katika kipindi cha pili, winga wa Uruguay 'Gonzalo Castro' alifumania nyavu na kuipa timu yake goli la kwanza. Castro alitwanga bao la pili baada ya Pique kupata kadi ya pili ya njano na kutolewa. Katika dakika za lala salama, Agirretxe aliteleza kumalizia mpira na kuwapa ushindi Real Sociedad wa 3-2. Hii ni timu ya tatu kutoa kichapo kwa Barcelona. Inaungana na Real Madrid katika 'Super Cup' ya Spain na Celtic kwenye 'champion league'.

Orange AFCON 2013 Yaanza Bila Magoli

Mashindano yalokuwa yakisubiriwa kwa hamu na shauku yamezizima nyoyo za washabiki walokuwa wakisubiri kuona timu kubwa kama Africa ya Kusini ikiicharaza Cape Verde katika mechi ya ufunguzi. Lakini mambo haya kuwa mambo, wanasema mtoto kakataa kutumwa dukani. Kalilia waende wote....Wachunguzi wa
masuala ya mpira wanasema ya kwamba yawezekana timu kubwa kama Afrika ya Kusini hawaja jiandaa vya kutosha "Wakidhania mpira ni lelemama" au Cape Verde walijiandaa kuikabili timu ya Mkongwa Nelson Mandela vilivyo. Wakitumia 'tactics' za kuharibu mpangilio wa pasi za mashambulizi ya Afrika ya Kusini. Kwa mtizamo wa wachambuzi hao ni

Hawa Ndio Yanga waliompiga Leopard 3-2

           Hawa ndio Yanga, wanna wa Jangwani. Wazee wa Ngamia.....Toka lini uliona chui akifanya mawindo jangwani? Jamani ukiona anajisifia sana ujue hana huyooooo......kitu empty set....mpaka ujiite Chui Mweusi Mwenye Makucha "Black Leopard's claws" inamaana kwani haijulikani kama Chui anakucha. Oooooh nshajua hizi kucha zao zitakuwa zimebandikwa kwa juu tu,zile za mapambo. Wana haki ya kuzisifia maana sio original.
Hii ilikuwa sababu tosha ya Black Leopard's claws kukubali kichapo cha bao 3 kwa 2. Warudi kwao Sauzi wakajifunze mpira. Mambo ya Uturuki hayo.....yeshaanza kuonekana. Wengine mjishike.........mjishike haswa!

Thursday, January 10, 2013

Who would you prefer to be the next signing for Man Utd

Frank Lampard (Chelsea)
Wilfried Zaha (Crystal Palace)
Wesley Sneijder (Inter Milan)
Luka Modric (Real Madrid)
Sven Bender (Borussia Dortmund)