Video and Shared space for ads

CF

Monday, March 26, 2012

Chezea Mnyama Wewe






Habarini mabibi na mabwana, Karibuni katika hii kona,
Jana wote tumeona, Mji ulizima kiaina,
Mnyama amenguruma,Ukitaka kujua waulize Setif,
Chezea Mnyama wewe;

Shangwe na vuvuzela zatanda kila kona za miji, Dar mpaka Rufiji,
Simba ndio magwiji, Wawafunika waarabu wa alaji,
Wawanywesha Setif vikombe vya uji, Viwili tu vyatosha kwa wao kurudi ujiji,
Chezea Mnyama wewe;

Hongera watoto wa Msimbazi, Okwi na Boban ndio mafundi,
Mmetupa raha za mkwezi, Kapanda mnazi katushushia kiufundi,
Poleni kwa wana-Setif wa juzi, kwa kupewa uji na mhindi choma,
Siku nyingine shangilieni tena kwa mbizi, tutawapa mpaka ndizi,
Chezea Mnyama wewe;


Ushauri kwa wachezaji, Tusibweteke na ushindi,
Tusilete ujuzi, na kudhania tuwashindi,
Tumeamua kuwaonyesha ugwiji, basi tujipange kiufundi,
 Chezea Mnyama wewe.
Imeandaliwa na Baharia

No comments:

Post a Comment